Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Kamati ya Uratibu ya Muqawama wa Iraqi imetoa tamko na kuzitaka taasisi za serikali na Bunge la Wawakilishi wa Iraq zitekeleze jukumu lao kupitia kamati husika kwa kusimamia hali ya majeshi ya uvamizi wa Kimarekani na kuyalazimisha kuondoka kwa moja kwa moja.
Kamati ya Uratibu katika tamko lake imesisitiza kuwa: Marekani muovu haitobadilisha siasa zake za uhasama dhidi ya wananchi, na haiwezi kuaminika katika ahadi zake wala katika hatua zake zenye shaka.
Katika tamko hilo limeelezwa: Majeshi ya Kimarekani yamepunguza idadi yao katika kambi na vituo vyao, lakini yameongeza ndege zisizo na rubani na ndege za kivita katika anga ya Iraq, na kwa kufanya hivyo yamezidi kukiuka mamlaka ya nchi yetu na kupuuza irada ya wananchi wetu.
Kamati ya Uratibu pia katika tamko lake imesisitiza kuwa: Mikono ya wanaume waaminifu wa Muqawama wa Iraqi bado ipo juu ya kitufe cha bunduki kwa ajili ya kulilinda taifa la Iraq, watu wake na vilevile Hashd al-Shaabi, ambayo Marekani na vibaraka wake katika eneo bado wanaendelea kuipinga.
Kamati ya Uratibu imewaomba Wairaqi kuhifadhi heshima ya wapiganaji wa Muqawama na kulinda maeneo ya vituo vyao, hususan kituo cha Saqar kinachohusiana na vikosi vya Hashd al-Shaabi.
Tamko hili mwishoni limeitaka Marekani ilazimishwe kuondoka kikamilifu na kuhakikisha mamlaka kamili ya Iraq juu ya ardhi na anga yake.
Maoni yako